MABINGWA wa ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga Alhamis watashuka katika dimba la Sheikh Amri Abeid mjini Tabora kuumana na Mtibwa
Sugar ya Morogoro.
Huo utakuwa mchezo wa tatu kwa Yanga ambayo ipo katika ziara
ya kimichezo Kanda ya Ziwa baada ya Jumamosi kutoka suluhu ya bao 1-1 na Express
ya Uganda
jijini Mwanza, kabla ya kufungwa 2-1 na Express katika mechi ya marudiano
iliyochezwa jana mjini Shinnyanga.