Msanii wa
muziki wa kizazi kipya ambaye amezidi kujijengea heshima ndani na nje ya nchi
Nasib Abdul maarufu kama Diamond anatarajiwa kupagawisha wakazi wa mkoa wa
Kigoma Jumamosi hii na style ya kipekee ya ‘Kikwetu Kwetu’ kwa hisani ya bia ya
Kilimanjaro.
Msanii
Diamond ataungana na wasanii wengine tisa wa muziki wa Bongo Fleva
watakaotumbuiza katika tamasha la ‘Kili Music Tour 2013’ ambalo linatarajiwa
kufanyika mjini Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika siku ya Jumamosi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager Bwana George
Kavishe alisema kuwa “tamasha la Kili Music Tour linaelekea Kigoma baada ya
kufanya vizuri jijini Mbeya, Mwanza, Dodoma, Tanga na Kilimanjaro. Wasanii kumi
ambao watatumbuiza Jumamosi hii ni Diamond Plutnumz, Linex, Barnaba, AT, Fid Q,
Prof J, Recho, Lady Jay Dee, Roma na Ben Paul.”
Bwana
Kavishe aliendelea kufafanua kuwa amefurahishwa sana na jinsi watanzania
wanavyopokea bonge la kiburudisho kutoka kwa bia yao ya Kilimanjaro. “ni faraja
kubwa kuona jinsi style ya “kikwetukwetu” ilivyokubalika nchini kote.
Kilimanjaro inaelewa fika kuwa watanzania wana mambo mengi sana ya kujivunia
ambayo ni ya kipekee kikwetukwetu. Ukiachana na bia ya Kilimanjaro Premium
Lager ambayo inatengenezwa Tanzania, na watanzania, kwa viungo vya kitanzania
kwa ajili ya watanzania, kuna mambo mengine mengi sana ya kikwetu kwetu kama
muziki wetu wa bongo fleva, dansi zetu za kiduku, kandanda letu na ushindani wa
Simba na Yanga, komedi yetu iliyo tofauti kabisa n.k. “
Kwa upande
wake Diamond alisema kuwa “Kama ilivyo kauli mbiu ya tamasha hili ‘Kikwetu
kwetu’ naamini nitatoa burudani kali kabisa kwa wanakigoma. Ukizingatia kuwa Kigoma ni nyumbani wanandugu
zangu wategemee bonge la kiburudisho kutoka kwangu na wasanii wenzangu nitakaokuwa
nao”.