Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya nembo yake ya Kilimanjaro Premium Lager, inangoa nanga kwa awamu ya pili ya ‘Kili Music Tour 2013’ wikiendi hii mjini Mwanza.
Matamasha ya Kili Music Tour 2013 yalikuwa yamepumzika kwa muda wa mwezi mmoja na yanarejea tena kwa kishindo kuanzia tarehe 17 Agosti, 2013 na baada ya hapo kuendelea kwenye mikoa iliyobaki.
Tamasha hili kubwa litafanyika Jumamosi ya tarehe 17 Agosti, 2013, mjini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba na litajumuisha wasaniii 11 ambao ni Diamond, Snura Mushi, Professor J, Lady Jay Dee, Roma, Dabo,Bob Jnr,Ben Pol, Kala Jeremiah, Fid Q,AT.
“Tunashukuru kuwa watanzania wamepokea tamasha hili kwa vizuri kabisa na wameshiriki kikamilifu kwenye mikoa ya Dodoma na Tanga na moshi, tuliamua kupumzika kwa mda wa mwezi mmoja ili kuboresha zaidi matamasha haya,hivyo basi tunategemea Mwanza itajumuika nasi ipasavyo kufanikisha tamasha litakalofanyika mkoani hapo Jumamosi ya tarehe 17.” Alisema bwana George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro
Bwana Kavishe aliendelea kufafanua kuwa “bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaendelea kutoa bonge la kiburudisho kwa watanzania kwa kuhakikisha kuwa kila mkoa unapelekewa wasanii mahiri kabisa wa muziki wa bongo fleva wawaburudishe “kikwetukwetu”