MICHEZO ya ligi kuu England baina ya Manchester United
dhidi ya Liverpool na ule baina ya Arsenal na Tottenham Hotspurs itakayopigwa jumapili imepelekea kusogezwa mbele kwa siku moja
mchezo wa kujipima nguvu baina ya Simba na Mafunzo ya Zanzibar.
Mchezo wa Simba
na Mafunzo uliokuwa ufanyike keshokutwa (jumapili) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
sasa utafanyika jumatatu katika dimba hilo kuanzia saa tisa alasiri.
Katibu Mkuu wa Simba Evodius Mtawala ameiambia SPORTS LADY BLOG kwamba wameamua
kuuslogeza mbele mchezo huo kutokana na maombi ya mashabiki wengi wa soka ambao
wametaka uahirishwe ili kupata fursa ya kuishuhudia michezo hiyo.
“Kama manavyojua mashabiki wa soka ndio wale wale hivyo
kutokana na jumapili kuwepo na mechi hizo mbili muhimu hivyo tumeona hatuna
budi kusikiliza maombi yao na kuusogeza mchezo huo,”alisema Mtawala
Aidha, mechi baina ya Simba na Mafunzo pia itatumika
kuwatambulisha nyota wa,ke wapya watatu Gilbert
Kaze, Amisi Tambwe kutoka nchini Burundi
na aliyekuwa nahodha wa zamani wa timu hiyo, Henry Joseph Shindika.
Kaze na Tambwe ambao itakuwa ni mara yao ya kwanza kuonekana kwa mashabiki wa jiji la Dar es
Salaam baada ya kukokekana katika tamasha la Simba Day lililofanyika Agosti 10
mwak huu kwenye Uwanja wa Taifa.
Huku kwa upande wa Henry, ambaye alikuwa akikipiga katika
klabu ya Kongsvinger ya Norway aliyojiunga nayo mwaka 2009 akitokea Simba,
amerejea tena nyumbani baada ya mkataba wake kumalizika mwezi uliopita.