TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni , uongozi wa Yanga uliitisha
mkutano Mkuu wa dharura uliokuwa
ufanyike tarehe 18 Agost 2013
viwanja vya sabasaba kwenye ukumbi wa PTA Saa 3:30 Asubuhi kwa lengo la
kujadiliana na suala la Azam Television kurusha mechi za Yanga. Mkutano huo kwa
sasa umeahirishwa kutokana na sababu
ifuatayo:
Tarehe 14.8.2014 Naibu Waziri wa Habari,
Utamadun,Vijanai na Michezo Mheshimiwa
Amosi Makala aliitisha kikao cha pamoja, kilichojumuisha pande zote husika
wakimwemo wasaidizi wake, shirikisho la
mpira wa miguu Tanzania(TFF),Mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi ya vodacom , uongozi
wa Yanga sc na uongozi wa Azam Media.
Baada ya kikao hicho yafuatayo ni makubaliano yaliyofikiwa
(a)Klabu ya Yanga itapata fursa ya kushiriki na kupitia
katika utengenezaji wa mkataba wa
udhamini wa haki za matangazo na televisheni
wa Azam Media ili kujiridhisha na vipengele vyote vya mikataba kwamba
kwa namna yoyote haviathiri klabu ya Yanga kufuatia uhusiano uliopo wa Azam
Media wanaotarajiwa kupewa haki hizo na Timu ya Mpira Azam FC moja ya timu pinzani ya Yanga kwenye
ligi ya Vodacom
(b)Kuwepo na utayari kwa uongozi wa Azam Media kukutana na
uongozi wa Yanga kuzungumzia mahusiano ya kibiashara yatakayo nufaisha pande
zote mbili.
Hivyo basi baada ya kuzingatia hayo uongozi unapenda kutoa
taarifa kwa wanachama wake kuwa mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 18 Agosti
2013, viwanja vya sabasaba kwenye ukumbi wa PTA Saa 3:30 asubuhi umeahirishwa
hadi mtakapotangaziwa vinginevyo, lengo ni kutoa nafasi na fursa kwa uongozi
kufanyia kazi hayo yaliyotajwa hapo juu
Pia uongozi unawashukuru wanachama na wapenzi wote wa Yanga
kwa kuonyesha ukomavu na kusimamia maendeleo
ya klabu yetu kwa Hali na mali , na uongozi Utaendelea
kusimama IMARA katika kuijenga Yanga Mpya
Uongozi pia unawataka wapenzi wote kuja kwa wingi uwanjani
kuishangilia timu yetu wakati wa mechi ya kugombea ngao ya hisani kuashiria
ufunguzi wa michuano ya kutetea ubingwa tunaoushikiria wa Ligi Kuu ya vodacom
Clement Sanga
Makamu Mwenyekiti
Young Africans Sports Club
16.08.2013