Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini
Naseeb Abdul ‘Diamond’ akifanya yake katika tamasha la Kili Music Tour
lililofanyika Kigoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Izzo
Bizness akiwapagawisha washabiki katika tamasha la Kili Music Tour
lililofanyika juzi kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Umati
wa mashabiki waliojitokeza kwenye tamasha la Kili Music Tour, wakifuatilia
onyesho hilo lililofanyioka kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Baadhi ya wasanii wa muziki nchini wakiwa pamoja na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
Msanii
wa muziki wa Hip Hop nchini Joseph Haule ‘Profesa Jay’ akitumbuiza katika
tamasha la Kili Music Tour Kigoma.
Diamond akiongoza wasanii wenzake
Mwasiti, Linex na Recho katika nyimbo ya ‘Leka Dutigite’ na kuwaamsha mashabiki
waliofurika uwanja wa Lake Tanganyika katika tamasha la Kili Music Tour, mjini
Kigoma.
Baadhi ya wasanii wa muziki nchini wakiwa pamoja na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
Na Mwandishi Wetu
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini,
Naseeb Abdul, juzi alifunika katika
tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini
Kigoma.
Katika tamasha hilo lililohudhuriwa na
umati wa mashabiki, Diamond alifanya onyesho la aina yake na kuwafanya
mashabiki kumshangilia kwa kupiga kelele.
Diamond ambaye alikuwa msanii wa mwisho
kupanda kwenye jukwaa, aliwaita wasanii wenzake ambao ndio wenyeji wa Kigoma
kama Recho, Mwasiti pamoja na Linex na kuimba wimbo wa Leka Dutigite na
kuwaamsha mashabiki waliofurika Uwanjani hapo.
Wasanii wengine ambao walitumbuiza
katika onyesho hilo lenye ujumbe wa ‘Kikwetu Kwetu’ ilikuwa ni pamoja na Lady
Jaydee, Barnaba, Ben Pol, Izzo Bizness, Recho, Prof. J, Fid. Q, Roma, Mwasiti,
Linex pamoja na Kala Jeremiah.