Na Dina
Ismail
KWA miaka
mingi Tanzania imekuwa ikifanya vibaya
katika michezo mbalimbali ya kimataifa ambayo inashiriki.
Licha ya
kujaliwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu lakini bado hali imekuwa
si ya kuridhisha kabisa.
Hata hivyo
sababu hasa ya kutokufanya vema na kujikuta kuwa wasindikizaji tu katika
mashindanio tunayojaliwa kushiriki bado haijajulikna.
Kwani kama
ni maandalizi hufanyika ya kutosha, kama ni walimu wapo wazuri sana iwe wazawa
ama wale wa kigeni ambao naamini hawana tofauti na wan chi nyingine.
Ukiangalia
kwa haraka haraka, kitu kikubwa kinachotukwamisha ni viongozi tulionao katika ngazi
mbalimbali.
Ndio!
Viongozi ndio kila kitu katika mafanikio ya kitu hivyo basi tunaweza kusema wao
ndio wanachingia tufanye vibaya au vizuri katika michezo.
Sifa ya
kiongozi bora ni kuhakikisha anasimamia vilivyo anachokiongoza ili mwisho wa
siku kiwe kitu bora na chenye manufaa kwa Taifa.
Na viongozi
wengi wa vyama vya michezo hawana sifa za viongozi kwani uwepo wao umetokana na
shinikizo kutokana na sababu fulani, ushabiki na mengineyo.
Kwamba wengi
wa viongozi katika michezo hawana wapo kwa manufaa yao binafsi na si katika
kuendeleza michezo.
Tumesshuhudia
katika kampeni kabla ya chaguzi mbalimbali, viongozi wengi wakitoa ahadi nzuri
sana na za kupendeza na kuwavutia wapiga kura lakini pindi wanapochaguliwa
hushindwa kutekeleza.
Hivyo basi,
kushindwa kwao kutekeleza ahadi walizoweka pindi wanaomba kura ndiyo inakuja
pelekeakubaki wasindikizaji katika michuano ya kimataifa.
Kiongozi
anaonekana kipindi cha kuomba kura tu na baada ya hapo humuoni ofisini wala
kwenye viwanja vya michezo kwa ajili ya kutoa sapoti ama neno lolote la faraja
kwa wanamichezo wa eneo lake.
Kiongozi
hajui hata wanamichezo ama michezo iliyopo katika eneo lake, yeye huishia kuja
kutoa pongezi kwa washindi au kuzindua mashindano tu.
Kuna maeneo
yamebarikiwa kuwa na hali nzuri ya hewa kwa ajili ya wanamichezo kufanya
maandalizi yao lakini kutokana na kuwa na viongozi wasiokuwa na kiu ya
mafanikio wanashindwa kuzitumia vema rasilimali hizo.
Ifikie
mahala wapiga kura wajiongeze kwa kuchagua viongozi ambao wana lengo na dhamira
ya dhati kabisa ya kuinua na kuendeleza michezo na si kuchagua viongozi ‘wauza
sura tu’.
Kwamba, kiongozi
anamwaga sera za kuvutia na anachaguliwa kwa kura nyingi, lakini anamaliza muda
wake bila kuleta mafanikio yoyote halafu anakuja kuomba tena nafasi ya
kuongoza, huyo hafai kabisa kurudi.
Kama kweli
tunataka mafanikio katika michezo ni vema wapiga kura kuchagua viongozi
wanaoona wana dhamira ya dhati na uchungu na maendeleo ya soka.
Pia kwa wale
viongozi maslahi ifikie mahala waone aibu kwa kujiweka kando na kuwaachia wenye
moyo wa dhati kuongoza.