Na Dina
Ismail
KUMEKUWA na
sintofahamu katika klabu ya soka ya Yanga kufuatia taarifa za kuwepo kwa hali
ya ukata unayoikabili.
Hali hiyo
inafuatia mwenyekiti na mdhamini wa timu hiyo, Yussuf Manji kuwa katika
misukosuko baada ya akaunti zake kufungwa na serikali.
Kwamba,
Manji baada ya kukumbwa na misukosuko hiyo klabu imekuwa katika hali mbaya ya
kifedha ambapo Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwassa akithibitisha hali
hiyo.
Kama hiyo
haitoshi, ukata huo umepelekea Yanga kusitisha ajira ya Mkurugenzi wake wa
ufundi, Hans Van Pluijim.
Pia kuna
taarifa ya baadhi ya wachezaji kwamba wapo mbioni kuikimbia klabu hiyo kutokana
na hali mbaya ya kiuchumi iliyonayo.
Hizi dalili
mbaya kwa klabu ya Yanga na isipochukuliwa tahadhari ni wazi kwamba itapoteza
hata matumaini yake ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara na
hata michezo yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga ni
mali ya wanachama hivyo basi ni wajibu kwa kila mwanachama mwenye mapenzi ya kweli kujitoa kwa hali na
mali kuhakikisha wanaiokoa klabu yao ili iweze kurudi katika mstari.
Kuendelea
kuacha jukumu la kuiendesha pekee kwa uongozi itakuwa ni kuwatwika mzigo ambao
hawawezi kuubeba.
Pia ni
wakati kwa viongozi kuamka katika usingizi wa muda mrefu iliokuwa imelala kwa
kutegemea mtu mmoja katika kuindesha kwenye masuala ya kiuchumi.
Yaangi,
viongozi wapigane kufa kupona ili kuhakikisha wanapatikana wafadhili ama
wadhamini ambao watamwaga fedha kwa ajili ya kuindeshe klabu hiyo.
Soka la sasa
lipo kibiashara zaidi, hivyo bila ya kuwa na fedha itakuwa gumu kwa klabu kubwa
kama Yanga kuishi kwa kutegemea mapato ya mlangoni tu.
Kwamba ,
tahadhari zisipochukuliwa ni mengi tutayasikia na kuyaona kwani Yanga
imesheheni wachezaji wa kigeni ambao wanahitaji kulipwa mishahara na stahiki
zao nyingine, hata wale wazawa pia wanahitaji kulipwa hivyo bila pesa kuna
kitakachochezwa hapo?
Tukirejea historia
ya soka la bongo inaonesha kwamba, dalili za namna hii na hasa kwa vilabu
vikubwa kama Yanga ni mbaya na zisipofanyiwa kazi zitawagharimu sana na
itawachukua muda mpaka kukaa katika mstari ulionyooka.
Yanga ambayo
pia inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika inahitaji kujiaandaa vema ili kuweza
kushinda michezo yake na kusonga mbele na maandalizi hayawezi kuwa bora bila ya
kuwepo kwa fedha.
Ni kipindi
ambacho ‘vivuruge’ watakitumia kwa lengo la kuhakikisha Yanga inaparaganyika
hivyo kushindwa kutimiza harakati zake za kutetea ubingwa.
Katika
kipindi hiki cha mpito ni vema kukawepo na amani na mshikamano ili mwisho wa
siku lolote litakalotokea libaki kuwa limetokana na umoja huo.
Bila
mshikamano ni wazi kwamba mtavuruga hadi akili za wachezaji wenu na hivyo
kupelekea kupoteza mwelekeo kabisa katika kutimiza wajibu wao .
Shime kwa
wanaYanga kuchukua tahadhari mapema kabla ya hatari kubwa inayioweza kuja
kutokea katika siku zijazo.