MBUNIFU maarufu wa mavazi na mitindo nchini Musatafa Hassanali yupo katika maandalizi ya mwisho ya onyesho lake lililobatizwa kwa jina la MAMA MIA linalotarajiwa kufanyika Machi 4 kwenye hoteli ya Movenpick na jingine la wazi litaklalofanyika Machi 5 katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Onyesho hilo lenye lengo la kuchangia kampeni ya utepe mweupe inayiojihusisha na uzazi salama kwa wanawake, pia litaambatana na uzinduzi wa mavazi mapya yaliyotayarishwa Hassanali.