ASHA BARAKA, MKURUGENZI WA ASET
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.AFRICAN STARS ENTERTAINMENT.
Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" Ijumaa ijayo inataraji kufanya onyesho maalum la kuchangia walioathirika na Mabomu ya Gongo la Mboto. Onyesho hilo linataraji kufanyika katika ukumbi wa Zhonghua Garden uliopo maeneo ya Victoria siku ya ijumaa tarehe 4-02-2011 na linataraji kuanza saa tatu za usiku. Matayarisho yote muhimu ya awali yameshaanza na Mgeni rasmi anatarajiwa kualikwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Jordan Rugimbana. Madhumuni ya ASET kuandaa ni baada ya kuguswa na kadhia iliyowapata maelfu ya wakazi wa Gongo la Mboto wengi wao kukosa makazi na kupoteza kila kitu hivyo kujikuta katika maisha mapya kabisa ambayo hawakuyategemea. hivyo ASET kupitia kwa bendi yake ya African Stars "Twanga Pepeta" imeamua kuchangia kwa kufanya onesho maalum ili kila atakayeingia kwa kulipa kiingilio cha tshs 5,000 basi kiingilio hicho kitaenda moja kwa moja kwa waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto. Ikumbukwe hapo awali ASET ilichangia walioathirika kwa mabomu kwa kutoa vitu mbalimbali, Lakini mchango huo umeona hautoshi hivyo ineamua kuandaa onyesho rasmi ili kupata fursa ya kupata michango zaidi toka kwa wapenzi na mashabiki wa Twanga Pepeta na wa Burudani kwa ujumla. Aidha ASET inataraji kuwaalika wadau wakubwa wa muziki wa dansi ili pamoja na mambo mengine kutafanyika Harambee na Mnada ili kupata fursa ya kupata michango toka kwa wadau ili iweze kusaidia waathirika wa mabomu. Kwa upande wa burudani, Twanga Pepeta imejiandaa vilivyo ili kutoa burudani kwa waalikwa watakaohudhuria kwenye onyesho hilo la kuchangia waathirika wa mabomu. Twanga Pepeta siku hiyo wataitambulisha singo yao mpya ya DUNIA DARAJA iliyotungwa na Charlz Baba.