SIKU CHACHE KABLA YA KUWAVAA YANGA, SIMBA YAPATA PIGO


SIMBA itamkosa kiungo wake wa kimataifa Hillary Echesa katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wa jadi Yanga itakayopigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Simba Clifford Ndimbo amesema kiungo huyon aliumia katika mechi yao na Mtibwa jumapili hivyo daktari amesema hatoweza kucheza mechi hiyo.
Alisema kikosi chote cha Simba kinaendelea na maandalizi yake visiwani zanzibar huku mchezaji wake mwingine wa kimataifa Joseph Owino naye aliyebaki jijini kwa ajili ya kuonana na daktari wake akitarajiwa kujiunga na wenzake wakati wowote.
Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Yanga iliyopigwa oktoba 16 katika dimba la kirumba jijini Mwanza, Yanga ilishinda bao 1-0.

Post a Comment

Previous Post Next Post