MABINGWA wa Tanzania Simba wameapa kulipiza kisasi cha kufungwa mabao 3-1 na wapinzani wao katika ligi ya Mabingwa barani Afrika Tp Mazembe ya Congo, mechi iliyopigwa jumapili katika jiji la Lubumbashi na Simba kuambulia kichapo cha mabao 3-1.Kocha wa Simba Patrick Phiri pamoja na wachezaji wamesema kupitia kipigo hicho watarekebisha makosa yaliyojitokeza ili kuweza kushinda mechi yao ya marudiano itakayopigwa wiki ijayo jijini dar es Salaam.