MWENYEKITI WA YANGA, LLOYD NCHUNGA
UONGOZI wa klabu ya Yanga ya jjijini Dar es Salaam umeamua kumuangukia aliyekuwa mjumbe wa bodi ya udhamini na mfadhili wa klabu hiyo Yussuf Manji ili kuinusuru na anguko la uchumi ambalo linaweza kuikumba klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa klabu hiyo , Llyod Nchunga, alisema, kikao cha Kamati ya Utendaji kilichoketi Februari 28 mwaka huu kimefikia uamuzi wa kumuangukia Manji, kutokana na kutambua mchango wake mkubwa aliokuwa akiutoa kwa klabu hiyo kupitia kampuni yake ya Quality Media Group na ufadhili katika usajili na masuala mengine yanayohusu timu.
Alisema Kamati hiyo ilisisitiza kufanyika kwa jitihada mbalimbali za kumrejesha mfadhili huyo kwa maelewano mapya ya kibishara ili kupanga namna ya kuendelea kuisadia klabu hiyo ambayo kwa mwaka inahitaji shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya kujiendesha.
Alifafanunua kuwa kiasi hicho cha pesa kinahusisha shilingi milioni 600 za usajili, milioni 50 kwa ajili ya mishahara ya wachezaji, benchi la ufundi, watumishi wa utawala na gharama za umeme na maji huku Yanga ikiingiza shilingi milioni 212.4 kupitia mkataba wa udhamini na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Nchunga alisema kupitia mchanganuo huo ni wazi Yanga inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mapato hivyo kiasi kikubwa cha fedha kilikuwa kikitolewa na Manji kwa takribani miaka mitano, hivyo nipigo kubwa kwa klabu hiyo kumkosa mfadhili huyo.
Alisema wakati jitihada za kumrejesha mfadhili huyo zikindelea uongozi wake umelazimika kubuni na kukaribisha vianzio vipya ikiwa ninmpamoja na akaunti maalumu kwa ajili ya mashabiki wa klabu hiyo ili kuweka amana.
Aidha Nchunga alisema, Kamati ya Utendaji imeridhia kupelekwa kwa majina yote ya wanachama wakorofi katika Mkutano Mkuu wa klabu ambao walihusika katika kutoa maneno ya kumfedhehesha Manji kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Alisema Kamati hiyO imeona kuna umuhimu wa Manji kuendelea kuidahili timu hiyo kutokana Yanga bado ilikuwa haijakomaa katika kujitegemea.
Hivi karibuni Manji alitangaza kujiondoa katika shughuli za klabu hiyo kutokana kitendo cha baadhi ya wanachama kumtolea maneno ya kashfa kabla ya uongozi wa klabu hiyo kumuangukia mara mbili kwa kumuandikia barua kumuomba abadilishe uamuzi wake lakini akagoma.