BENDI ya Extra Bongo kwa mara nyingine tena imeibomoa The African Stars 'Twanga Pepeta' baada ya kumnyakua mnenguaji wake mahiri Aisha Mohamed Madind, ambapo leo mkurugenzi wa Extra Bongo, Ali Choki amemtambulisha Madinda kwa waandishi wa Habari.
Choky alisema Madinda amejiunga na Extra kwa matakwa yake mwenyewe , na tayari ameshaanza mazoezi na bendi hiyo wiki mbili zilizopita.