KUNDI la muziki wa taarabu nchini la Jahazi Modern Taarab linatarajiwa kufanya onyesho maalum kwa ajili ya kuukaribisha mwezi wa mtukufu usiku wa Julai 29 katika ukumbi Savoi, mjini Morogoro.
Mratibu wa onyesho hilo, Said Mdoe alisema lengo ni kuwapa raha mashabiki wa huko na hasa ikizingatiwa kuwa baada ya hapo mfungo wa ramadhani utabisha hodi.
Alisema ili kuongeza nakshi za onyesho hilo, pia kundi maarufu la unenguaji la Kanga Moja Ndembe ndembe nalo litasindikiza ambapo litamiliki jukwaa kwa mitindo tofauti ya unenguaji.