MASHABIKI MBEYA WAZIPONDA SIMBA, YANGA


LICHA ya  timu za soka Simba na Yanga kutinga nusu fainali katika michuano Kagame Castle cup inayoendelea kutimua vumbi katika uwanja wa Taifa jijini Dar-es-Saalam,  wadau mbalimbali hapa  wameonyesha kutoridhishwa na kiwango ilichonacho timu hizo. 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi mara baada ya kumalizika kwa mechi baina ya Yanga na Red Sea  mmoja wa wanachama wa  Yanga Benson Mwakasege alisema licha kuwa wenyeji wa micchuano hiyo,  timu zote  zimeonyesha kiwango cha chini  tofauti na matarajio ya  wengi. 
Mwakasega ambaye pia ni  mchezaji wa zamani wa timu ya kampuni ya wafanyabiashara mkoa wa Mbeya (RTC) kuwa timu ya Simba pekee ndiyo angalau iliweza kuonyesha uhai katika michuano hiyo na imekuwa ikiiimarika kadiri siku zinavyosonga. 
'Mimi ni mwanachama halali wa Yanga na  kadi  yangu nimeacha nyumbani lakini lazima niwe mkweli kiwango kilichoonyeshwaa na klabu zetu zote mbili sio cha kuridhisha licha ya kwamba kutinga kwao nusu fainali lakini wao bado sana hivyo  tunahitaji maandalizi ya kutosha,” alisema Mwakasege. 
Aliongeza kuwa, inashangaza kuona msinmu wa usajili umemalizika hivi karibuni lakini wachezaji hawonyeshi kiwango cha kuweza kuwavutia wapenzi na washabiki wa soka hapa nchini, pia wachezaji wengi wa sasa hawajitumi licha kupewa huduma stahiki. 
Naye mfanyabiashara maarufu mjini Tunduma Sulemani Tweve mabaye ni shabiki wa simba  alisema kuwa timu zote mbili zimeonyesha kiwango cha chini hasa nafasi ya kiungo na kuongeza kuwa mpira wa  wa siku hizi na wakisasa zaidi na kama  timu haina viungo wenye kasi na kuweza kumiki mpira basi haiwezi kufika mbali katika mashiondano yoyote. 
Wakati  Simba ilitinga nusu fainali baada ya kuibamiza timu ya Bunawaya Uganda kwa mabao 2-1, Yanga ilitinga hatua hiyo baada kuondosha Red Sea Eritrea kwa changamoto ya mikwaju 6-5.

Post a Comment

Previous Post Next Post