KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Kim Poulsen, jana ameweka wazi majina ya kikosi cha wachezaji 30 aliowateua kupitia timu mbalimbali zilizokuwa zikishiriki katika mashindano ya Copa CocaCola na ile ya shule za Sekondari (UMISETA).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Poulsen alisema kuwa kikosi hicho kitakuwa kikifanya mazoezi katika uwanja wa Karume kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa.
Huku Mabeki ni Ismail Adam(Kigoma united),Miraji Adam(Mwele Kids, Morogoro), Hamidu Juma(Kigoma United) na Mohamed Husein(Friends Rangers, Kinondoni).
Viungo ni Paschal Abid(Dodoma), Mgaya Abdul(KifaUnited),PauloJames(Ambasader, Shinyanga),James Ambros,Amon Izak (Mkamba, Morogoro),Abbas Peter(Veteran, Tanga), Mudathiri Yahya, (Orange, Mjini Magharibi), Maulid Mohamed(Kombora,Temeke), Mohamed Salum(Arizona,Mjini Magharibi),Faridi Musa(Amani, Kilimanjaro,Hussein Twaha(Makororora, Tanga), Mbwana Ilyasa(Champion, Tanga na Mbwana Charles(Kinondoni).
Kwa upande wa washambuliaji ni Yunus Benard(Orange, Mjini Magharibi), Ahmed Abbs(Friends, Kinondoni), Awadh Athumani(Alikadiri,Temeke), Joseph Kimwaga(Villa Squad, Kinondoni), Ismail Moba(Vijana Ilala,Kigoma), Tumaini Venance, Innocent Nikolaus (Amani center, Kilimanjaro),Gadson Nyamtema(Vijana, Kasulu)Salvatory Raphael(Red Star, Kigoma) na Basil Abdul(Kihonda Morogoro).
Wachezaji wengine ni pamoja na Juma Botu(Makongo, sekondari),Mpesya(Nyanda za Juu) Mbeya na Aron Ally(Mpwapwa sekondari).