MABINGWA mara tatu wa kombe la Kagame Castle Cup, Yanga, leo wametinga nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga kwa penati Red Sea ya Eritrea katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam .
Yanga iliyotwaa kombe hilo mwaka 1975, 1995 na 1999 sasa watakutana na St.George ya Ethiopia ambayo iliitoa Vital’O ya Burundi kwa mabao 2-0katika mechi ya kwanza ya robo fainali iliyopigwa mchana wa leo.
Shujaa wa Yanga jana alikuwa Nurdin Bakari aliyefunga Penati ya mwisho baada kipa wa Yanga Yaw Berko kupangua mikwaju sita kati ya saba za Red Sea hivyo kufanya Yanga kuibuka na ushindi wa 6-5
Mwamuzi, Sylvester Kirwa wa Kenya aliamuru hatua ya penati baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa suluhu ya bila kufungana.
Shadrack Nsajingwa, Keneth Assamoh, Rashid Gumbo, Davies Mwape, Nadir Haroub na Nurdin Bakari walipata kwa upande wa Yanga huku Kigi Makasi akikosa.
Kwa upande wa Red Sea , waliopata ni Temesgen Asefaw, Yakob Takie, Kibron Andemariam, Daniel Ogbagabriel na Daniel Gaitom, huku waliokosa ni pamoja na Henok Berhe na Abraham Tedros.
Katika mechi hiyo iliyokuwa na upinzani mkubwa kwa timu kushambuliana kwa zamu, katika dakika ya 7 mshambuliaji wa Yanga Davies Mwape alipokea pasi ya Rashid Gumbo na kushindwa kufunga akiwa ndani ya 18 baada mpira wake kudakwa na kipa wa Red Sea .
Dakika ya 36 abraham Tedros wa Red Sea alipokea pasi ya Yakob Tekie na kupiga mpira uliopaa juu ya lango la Yanga, wakati ira uliopita juu ya lango la Yanga,.
Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano hiyo, Simba wao watakuwa na kibarua kizito kesho watakapolwaana na El Mereikh ya Sudani katika mchezo wa nusu fainali wa michuano hiyo.
Yanga:Yaw Berko, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Julius Mrope, Oscar Joshua, Chacha Marwa, Nadir Haroub, Nurdin Bakari, Rashid Gumbo, Davies Mwape, Hamisi Kiiza/ Kenneth Assamoah na Kigi Makasi.
sasa ulitaka nini kiebebe yanga..acha unazi wa simba bana mbona jana ulinadika werawera simba . leo matuta yaibeba yanga... najuwa wewe nimpenzi wa simba tu..ukatae ubishe.....mimi ni shabiki wa timu ya lipuli...
ReplyDelete