SEKONDARI YA GOBA YAANZA VEMA MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS

SHULE  Secondari ya Goba ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam imeanza vema  michuano ya vijana wenye umri  chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kuichapa shule ya Mpijimagohe kwa mabao 3-2,  kwenye mechi kali iliyochezwa kwenye uwanja wa Makongo Secondari jana.
 Mechi hiyo ni moja kati ya michezo mitatu ya ufunguzi wa mashindano hayo inayoshirikisha jumla ya timu 24 za shule za sekondari  kutoka mikoa ya K’ndoni, Ilala, Temeke, Morogoro, Iringa na Mwanza.
Katika mechi ya jana, mchezo ulianza taratibu huku kila timu ikicheza mchezo wa kujilinda zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza. Hata hivyo, ilikuwa ni Mpijimagohe ambao walionekana kumiliki zaidi mpira kwani iliwachukua dakika tano tu kuanza kufanya mashambulizi  langoni mwa  wapinzani wao. Mnamo dakika ya tisa ya mchezo, timu ya Goba walifanya shambulizi na kujipatia bao la kwanza lililowekwa kimiani na Jumanne Rashid. Kabla ya kufunga bao hilo, mfungaji  alipata pasi akiwa nje kidogo ya eneo la hatari na kuwalamba chenga mabeki watatu wa Mpijimagohe na kisha kuukwamisha mpira wavuni.
Kufuatia bao hilo, Goba waliamka na kuanza kumiliki sehemu kubwa ya mchezo, huku wakicheza pasi za uhakika na kuwashangiliwa sana na mashabiki waliohudhuria mchezo huo.Bao la pili la Goba lilipatikana  dakika ya 25  kufuatia mpira free kick iliyopingwa kutoka wingi ya kulia na mpira kumkuta Momahammed Seif aliyekuwa katika nafasi nzuri na kuukwamisha mpira wavuni.
Baada ya kuingia kwa bao hilo, shule ya Mpijimagohe ilifanya mabadiliko ambapo Juma Mtoro aliingia akichuka nafasi ya Gervis Mwinje. Hata hivyo, mabadiliko hayo hayakubadilisha mchezo kwani hadi timu zionakwenda mapumziko  Goba ilikua mbele kwa bao 2-0.
Kipindi cha pili Mpijimagohe walifanya mabadiliko mengine ambapo Mohammed Shabani alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Issa Rajab. Goba iliendelea kumiliki sehemu kubwa ya mchezo na katika dakika 54 ilifanikiwa kupata bao la tatu kupitia tena kwa  Jumanne Rashid  ambaye kabla ya kufunga aliwalamba chenga mabeki wa Mpijimagohe waliodhani ameotea. Dakika ya 67 Mpijimagohe walifanya mabadiliko mengine ambapo Ibrahim Juma alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Livingstone Shayo.
Kuingia kwa bao hilo kuliwafanya Mpijimagohekuzinduka na kuanza kusukuma mashambulizi langoni mwa wapinzani wao na kufanikiwa kujipatia bao la kwanza kunako dakika ya  68 mfugaji akiwa Juma Haruna kufuatia piga nikupige  langoni mwa Goba. Baada ya goli hilo waliendelea kulishambulia lango la Goba kama nyuki na dakika ya 77 wakaongeza bao la pili mfungaji akiwa ni Mohammed Shauri, ambapo aliwazindi mbio mabeki wa Goba na kuanchia shuti kali na kutinga wavuni moja kwa moja. Mpijimagohe waliendelea kumiliki sehemu ya mchezo lakini mpaka filimbi ya mwisho ya mchezo Goba ilitoka kifua mbele kwa mabao 3-2.
Katika mechi nyingine ya michuano hiyo kwa wilaya ya Temeke iliyochezwa kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kurasini, Shule ya Sekondari ya Jitegemee ilifunga shule ya Kubugumo

Post a Comment

Previous Post Next Post