WEKUNDU wa Msimbazi, Simba leo jioni wanatarajia kuanza mazoezi ya uwanjani kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania bara inayotarajia kuanza Agosti.
Mazoezi ya Simba ni kwa maandalizi ya Simba Day inayotarajia kusherehekewa Agosti 8 sambamba na mechi ya Ngao ya Hisani itakayochezwa Agosti 13.
Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema mazoezi ya Simba yanaanza baada ya kocha Mkuu, Moses Basena kuwasili juzi kutokea mapumzikoni nchini Uganda.
Kamwaga alisema kabla ya mazoezi ya pamoja ya jioni, asubuhi Simba watafanya mazoezi ya Gym ambayo walianza tangu Alhamis iliyopita.