SERIKALI YAMLIPA KOCHA HEWA NETIBOLI


IMEBAINIKA kuwa, serikali imeanza kumlipa Kocha wa Taifa wa Netiboli, Simone Macknnis ili hali akiwa amekwishafungasha virago kurejea kwao Australia.
Kocha huyo ambaye alikuja nchini kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete, ambako Desemba mwaka jana aliamua kuvunja mkataba kutokana na kutotekelezwa vema, ikiwamo kucheleweshewa mishahara, malazi na usafiri na serikali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi alibainisha kuwa, serikali kupitia Wizara husika na michezo, ilitoa fedha za kununua gari kwa ajili ya kocha huyo, Februari mwaka huu wakati Simone tayari kishabwaga manyanga.
“Inashangaza, hata kulipia kodi ya pango na mishahara wamelipa tayari Kocha kaondoka, ndio maana hata mishahara ya miezi miwili aliamua kuirejesha, kwani hakuifanyia kazi,” alifafanua Bayi.
Kuhusu gari, alisema serikali iliwatumia fedha kwenye akaunti yao na tayari limenunuliwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post