VIONGOZI wa klabu ya soka ya Simba wanatarajiwa kwenda nchini uturuki kwa ajili ya kumalizia taratibu za ujenzi wa uwanja wake mpya wa kisasa uliopo Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kampuni ya Petroland ya huko ndiyo imepata tenda ya kujenga uwanja huo ambao pindi utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuchuakua watazamaji 60,000 walioketi, pia utakuwa na kumbi za burudani, hoteli, mikutano, maduka, vituo vya michezo n.k.
Awali wawakilishi wa Petroland walikuja nchini kwa ajili ya kufanya tathmini ya uwanja huo ambao unatarajiwa kugharimu bilioni 75 za Kitanzania pindi utakapomalizika.
Tumechoka na ahadi hewa, wanaenda kutalii hao. Hakuna cha uwanja wala nini, maneno tu. Klabu ni Azam hawaongei kwa maneno wanafanya kwa matendo. Ndio sababu hata magazetini hawaandikwi sana sababu waandishi wengi ni Simba au Yanga.
ReplyDelete