SIMBA YAWAZODOA KINA BANKA


KLABU ya Simba imesema haitabadi msimamo wake dhidi ya wachezaji iliowapeleka kucheza kwa mkopo katika klabu nyingine za Ligi Kuu Bara katika msimu ujao utakaoanza Agosti 20.
Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wachezaji kugoma kuhamishwa wakidai kutoshirikishwa kwenye mpango huo huku Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) nalo likidai kuwa kitendo walichofanyiwa na klabu si cha kiungwana.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ (PICHANI) alisema kitendo cha wachezaji kugoma kujiunga na klabu walizopelekwa kwa mkopo, ni sawa na kugoma kuichezea Simba.
Alisema, maamuzi ya kuwahamisha yalitolewa na kocha wao mkuu Moses Basena huku wachezaji husika wakiitwa na kutakiwa kutaja klabu ambazo wangependa kujiunga nazo kwa mkopo na kuelezwa kuwa, kinyume na hapo wangepelekwa katika timu yoyote.
“Tuliwataarifu na kuna wengine akiwemo Shiboli (Ali Ahmedi), walifanya mawasiliano na timu nyingine na wakabubaliana, sasa nashangazwa na baadhi yao kulalamika katika vyombo vya habari kama hawakutaarifiwa juu ya suala hilo,” alisema.
Kaburu aliongeza kuwa, pamoja na kupelekwa huko wachezaji hao bado ni halali katika klabu ya Simba na kama hawatokuwa tayari kuzitumikia timu walizopelekwa, ni sawa na kuvunja mkataba wao wenyewe.
Wachezaji waliotolewa kwa mkopo kutoka Simba kwenda klabu zingine ni Aziz Gilla na Mbwana Bakari (Coastal Union), Mohammed Banka, Mohamed Kijuso na HarunaShamte.

Post a Comment

Previous Post Next Post