MABINGWA wa klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama ‘Kagame Cup’ mwaka 2011, timu ya soka ya Yanga inatarajiwa kwenda mjini Dodoma kesho kwa ajili ya kupeleka Kombe la Ubingwa kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mratibu wa ziara hiyo maalum Cellina Agustino, lengo la ziara hiyo ni pamoja na kuwapa nafasi wabunge hao kulishuhudia pamoja na wakazi wa mkoa wa Dodoma .
Alisema, wachezaji wa Yanga kesho watatinga katika bunge na kisha baadaye kujumuika na wabunge katika tafrija fupi waliyoandaliwa.
“Mara baada ya tafrija fupi, wachezaji wa Yanga jioni watafanya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Jamhuri na keshokutwa Jumamosi watakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Polisi Dodoma, “alisema .
Alisema kuwa maandalizi ya kila kitu kimekamilika ambapo Yanga ittakuwepo mkoani humo kwa muda siku nne na kurejea Dar es Salaam siku ya Jumapili.