YANGA KICHEKO WAENDA DODOMA KESHO

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzabnia Bara, Yanga wanatarajia kwenda mjini Dodoma kesho tayari kwa mechi yake ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu bara dhidi ya Polisi Dodoma utakaopigwa Jumatano katika dimba la Jamhuri mjini Dodoma.
Yanga inakwenda huko ikiwa na nguvu zaidi kutokana na kufanikiwa kuvunja mwiko wa mahasimu wao wa jadi nchini Simba kutofungwa tangu kuanza kwa ligi hii, pale walipoifunga jumamosi bao 1-0.
Ofisa habari wa Yanga, Louis Sendeu amesema kwamba wachezaji 20 na viongozi watano watakuwem,o katika msafara huo na kwamba kikosi chake kipo katika hali nzuri.

Post a Comment

Previous Post Next Post