RAGE AZIAGIZA KAMATI KUTOA TAARIFA ZA MECHI YAO NA YANGA

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
MARA baada ya mechi ya watani wa jadi ya Ligi Kuu ya Tanzania (VPL) Jumamosi iliyopita, kumeibuka matukio na taarifa nyingi na klabu imeamua kutoa tamko rasmi kuhusiana na pambano hilo.
La kwanza ni kuwa uongozi, benchi la ufundi na wachezaji wote wa Simba Sports Club (SSC), wamesikitishwa sana na matokeo ya pambano hilo dhidi ya Yanga. Kwa taarifa hii tunapenda kuomba radhi ya dhati kabisa kwa wana Simba wote ambao tunafahamu wameumizwa sana na matokeo hayo.
Kutokana na matokeo hayo, Mwenyekiti wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage (Mb) ameziagiza kamati mbili za SSC –ya Ufundi na Mashindano, kukutana haraka na kuandaa taarifa kuhusu mwenendo mzima wa klabu katika msimu huu na pambano hilo la watani wa jadi.
Pia, Mwenyekiti amemuagiza Kocha Mkuu wa SSC, Moses Basena, kuandaa ripoti kamili kuhusu timu na kuiwasilisha kwake kabla ya Ijumaa wiki hii.
Mwenyekiti wa Simba ataziwasilisha ripoti hizo; za kamati na ya mwalimu, kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji kilichopangwa kufanyika Ijumaa wiki hii jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliwa.
Kamati ya Utendaji ya klabu itafanya maamuzi yake kutokana na ripoti hizo za kamati.
Kwa taarifa hii, SSC inawaomba wanachama wake kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu kwao. Ule mmoja na ushikamano uliokuwapo wakati wa kuelekea katika pambano la watani wa jadi unatakiwa kuendelea kuwapo ili kuzuia maadui wasituvuruge.
Bado kuna mechi ya kucheza kabla ya kumalizika kwa raundi ya kwanza ya Ligi Kuu. Kama Simba itashinda mechi hiyo dhidi ya Moro United, itajihakikishia kuongoza ligi hadi mwakani wakati raundi ya pili itakapoanza.
Uongozi unaomba wachezaji na wanachama kuhamisha mawazo yao yote katika pambano hilo haraka iwezekanvyo. Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.

Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Msemaji
Simba Sports Club

3 Comments

  1. HAMNA LOLOTE SIMBA MMETANDIKWA HATA MUWEKE VIKAO KIVYENU TUMEWACHINJA NA KUWALA NYAMA YENU BASI KWISHINE MKIJA JIULIZA TUNAWATANDIKA TENA MAWILI HAPO SASA HAHAHAHA OYA OYA SIMBA YANGA KIBOKO YENU Mdau richie yanga damu wa ughaibuni

    ReplyDelete
  2. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHNovember 1, 2011 at 3:02 AM

    BADO MNAWEWESEKA TU NA KIPIGO??SIE TUMESHASAHAU

    ReplyDelete
  3. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHNovember 1, 2011 at 8:21 PM

    HIZO NI KAMATI ALIZOZIAGIZA ADEN NI KWA AJILI YA KUSHUGHULIKIA TARATIBU ZA MAZISHI YA MAREHEMU MNYAMA SIMBA YALIYOSABABISHWA NA KUVUJA DAMU NYINGI BAADA YA KIPIGO CHA JMOSI

    MDAU WA YANGA BOMBA-GRAND RAPIDS,USA.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post