MKE wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal (pichani kushoto), anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi rasmi wa kundi jipya la Taarab na albam ya kwanza ya kundi hilo, ambalo kwa sasa limekuwa gumzo kubwa kwa mashabiki wa muziki wa Taarab Nchini, Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ama Real Madrid.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini, alisema kuwa uzinduzi wa kundi hilo ulisogezwa mbele hadi kesho Ijumaa, badala ya tarehe ya kwanza iliyokuwa imepangwa ya oktoba 28, kutokana na ukumbi huo kuwa na shughuli ya ghafla ya Waziri Mkuu katika tarehe hiyo iliyokuwa imepangwa kufanyika uzinduzi huo.
Aidha Amini alisema kuwa baada ya ratiba hizo kuingiliana katika ukumbi huo mmoja wa Diamond Jubilee, ilibidi kundi hilo kusitisha na kusogeza mbele uzinduzi wake ambapo kwa sasa maandalizi yote kuhusu uzinduzi tayari yamekamilika.
Amini alivitaja vikundi vitakavyosindikiza onyesho la uzinduzi huo kuwa ni pamoja na Bendi mahiri inayoundwa na vijana watatu, Mapacha wa3, Bendi kongwe nchini, Msondo Ngoma, Sabaha Salum, anayeimba miondoko ya Taarab pamoja na Kikundi cha Sanaa cha Twins Voice, kinachoimba nyimbo za kuhamasisha kujilinda dhidi ya magonjwa ya Ukimwi.
Pia Amini alitaja viingilio vya onyesho hilo kuwa mashabiki wote wataingi ukumbini kushuhudia onyesho hilo kwa kulipa sh, 10,000 tu, ambapo pia baada ya uzinduzi huo zitapatikana Kanda za albam hiyo zitakazokuwa zikiuzwa ukumbini humo.