PAPIC ACHEKEA USHINDI WA POLISI, AWAPA WACHEZAJI MAPUMZIKO YA WIKI TATU

KOCHA wa Yanga, Kostadin Papic ameeleza kufurahishwa na ushindi wa bao 1-0 iliyoipata jana dhidi ya Polisi Dodoma, katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara uliopigwa mjini Dodoma.
Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 27 ambazo zinawaweka katika nafasi ya pili nyuma ya mahasimu wao wa jadi Simba.
Akizungumza mara baada ya kurejea toka Dodoma leo, Papic alisema matokeo hayo yanampa mwanga wa kuendeklea kufanmya vema kwenye ligi hiyo na hatimaye kutwaa tena ubingwa kwa mwaka huu.
Aliongeza kuwa, wachezaji wa timu hiyo watakwenda katika mapumziko ya wiki tatu ili kupisha maandalizi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mechi yake ya kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya Chad.

Post a Comment

Previous Post Next Post