TIP KUFANYA BONGE LA PARTY KUSHEREHEA KUTIMIZA MIAKA 10

KUNDI la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam linatarajiwa kufanya sherehe ya kutimiza miaka kumi ya uhai wake kwenye game.
Meneja wa kundi hilo Babu Tale amesema leo kwamba wanatarajia kufanya sherehe za kufa mtu Jumapili ya Novemba 13 katika ukumbi wa Maisha Club ambapo kutakuwa na burudani toka kwa wasanii mbalimbali.
Wasanii waliopo katika kundi hilo lililopata kuibua nyota kama Keysha, Mb Dog, Z-Anto na Spark, ni pamoja na Madee, Tundaman, Richard, Deso na Dogo Janja.

Post a Comment

Previous Post Next Post