MMMOJA ya washindi washindano la Tusker All Stars 2011 Peter Msechu, amewaomba radhi Watanzania na mashabiki wa muziki wake kwa ujumla kutokana na kuvaa nguo zilizoonyesha nguo zake za ndani (mlegezo), siku ya fainali za shindano la Bongo Stars Search (BSS Second Chance 2011) zilizofanyia kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Msechu amesema hakukukusudia kuvaa vile bali wakati akijiandaa kupanda jukwaani kwa bahati mbaya kifungo cha kaptula aliyovaa kukatika na hivyo kufanya ishuke chini ya makalio.
"Najua kuna baadhi ya watu nimewakweza, lakini nawaombeni radhi sana kwani halikuwa kusuadio langu,"Alisema.
Msechu anatarajia kuachia video ya wimbo wake uitwao 'Relax'.