VIBOPA YANGA KUSITISHA MISAADA IWAPO...


Na Dina Ismail
BAADHI ya matajiri wa klabu ya soka ya Yanga wamesema watasitisha kutoa fedha kwa wachezaji wa klabu hiyo kama motisha iwapo uongozi utaendelea na msimamo wa kutaka fedha hizo zipitie mikononi mwao.
Hatua hiyo inafuatia viongozi wa Yanga kuzuia shilingi milioni 10 zilizotolewa na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Davies Mosha wiki iliyopita akitimizxa ahadi aliyotoa ya kuwazawadia baada ya kuwafunga mahasimu wao, Simba bao 1-0.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao, matajiri hao ambao wamekuwa wakiisaidia timu hiyo, waliliambia gazeti hili jana kwamba, wanatoa fedha hizo kwa wachezaji kwa mapenzi yao lakini wanapata wasiwasi na kitendo cha vingozi kutaka fedha ziwafikie wao kwanza.
Walisema wanashindwa kuelewa kuna siri gani inayopelekea viongozi kutaka fedha hizi zifike kwao na ndipo wazigawe kwa wachezaji kitu ambacho katika hali ya kawaida hakiwezi kukubalika.
“Jamani mimi nimeamua kutoa fedha kwa ajili ya kuwapa wachezaji na si klabu sasa kwa nini nizipeleke kwanza kwa viongozi tena kwa siri na ndipo wawapatie wachezaji, hayo ni mambo ya kizamani ambayo hayanabudi kuendekezwa,”alisema mmoja ya matajiri hao.
Akizungumzia hatua hiyo, mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga na mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Ahmed Seif aliwataka matajiri hao kutokatishwa tamaa na kauli ya katibu wa Yanga, Selistine Mwesigwa aliyoitoa hivi karibuni baada ya Mosha kutoa fedha hizo na kusema kuwa mtu byoyote anayetoa heka kwa wachezaji anatakiwa kuzipeleka kwanza kwa viongozi.
Seif alisema yupo tayari kuwapa uishirikiano matajiri hao iwapo watataka kutoa msaada wowote kwa wachezaji milango ipo wazi.

Dalili za fedha za mosha kuleta utata zilianza kuonekana siku zilipopelekwa ambapo uongozi ulionekana kutopenda kuendeshwa kwa zoezi hilo lakini baada ya kugundua kuwa njama zao hizo zilijulikana kwa waandishi wa habari waliruhusu baa\dhi ya wachezaji kuwawakilisha wenzao ambapo pia zoezi hilo lilihudhuriwa na mjumbe wa kamati ya utendaji Ali Mayai na kocha wao, Kostadin papic.

1 Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHNovember 8, 2011 at 7:06 PM

    BWANA "mmoja ya matajiri" ACHA MAJUNGU YANGA IMETULIA KWA SASA,WE MWENYEWE ULIANDIKA BARUA YA KUJIUZULU SASA CHOKOCHOKO ZA NINI TENA?YANGA NI TAASISI LAZIMA MAMBO YAENDE KWA MPANGILIO HATA HUYU SWAHIBA WAKO SEIF NI KIONGOZI WA YANGA MTUMIE HUYO KAMA SHIDA YAKO NI KUTOKUBALI KUONA UNAFANYA MAMBO YA YANGA CHINI YA LOYD NCHUNGA AMBAE NI MWENYEKITI WETU HALALI TULIEMCHAGUA!KAMA NIA YAKO NI NJEMA MBONA HUTAJI JINA HAPA UNAISHIA KUJIITA ETI "MMOJA WA MATAJIRI" HALAFU KWA NINI YANGA INAPOFANYA VIBAYA INAKUA YA NCHUNGA IKIFANYA VIZURI KILA MTU ANATAKA KUWA FRONT AONEKANE YUPO NYUMA YA MAFANIKIO?????ACHENI KUTAFUTA CHEAP POPURARITY KWA MIGONGO YA WENGINE,KWANINI MLIJIUZULU SI MLITEGEMEA LOYD AHADHIRIKE KAMA MWENYEKITI SIO,SASA MUNGU ANA MAMBO YAKE YEYE AMEINGIA KWENYE RECORD YA WENYEVITI WA YANGA WENYE MAFANIKIO,CHINI YA UONGOZI WAKE MATAJI YAMEKUWA YAKIMIMINIKA JANGWANI YAKIWEMO YA KIMATAIFA!!HAKUNA ATAKAEWEZA KUFUTA HISTORIA HIYO KWA KUGAWA MILIONI KUMI KIHOLELA KWA WACHEZAJI!HIZO MILIONI KUMI NANI ATAZIKUMBUKA???WATU WATAMKUMBUKA MWENYEKITI ALIEKUWAPO MADARAKANI KIPINDI CHA MATAJI HAYA!NYAMBAFF...!

    MDAU WA YANGA BOMBA,MICHIGAN STATE,USA.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post