MABINGWA wa ligi kuu soka TAnzania Bara, Yanga wamewasili mjini Dodoma tayari kwa mechi yao ya ligi hiyo dhidi ya maafande wa Polisi Dodoma utakaorindima kwenye dimba la Jamhuri Mjini Dodoma.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu amesema kwamba kikosi chake kimewasili salama na jioni hii kinafanya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo utakaokuwa na ushindani mkubwa, huku akijinasibu ya timu yake kushinda na kujipatia pointi tatu.
Mechi nyingine kesho ni Oljoro JKT vs Villa Squad (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid)
Toto Africans vs Azam (Uwanja wa CCM Kirumba)
Mtibwa Sugar vs African Lyon (Uwanja wa Manungu)
Ruvu Shooting vs JKT Ruvu (Uwanja wa Mlandizi)
SISI SASA HIVI NI MBELE KWA MBELE,WE MAMA SIMBA NASIKIA MMEANZA KUFUKUZANA TENA LICHA YA MSEMAJI WENU JANA KUKANUSHA UGOMVI NA KUSEMA HALI NI SHWARI...HEBU TUMWAGIE TAARIFA HAPA ACHA KUBANA MAMA EEH,KUNA HABARI NIMEINASA SASA HIVI KUTOKA HUKO BONGO INASEMA:
ReplyDelete"Klabu ya simba leo imemfuta kibarua kocha wao Moses Basena baada ya kufungwa na Yanga bao 1 - 0 katika mchezo wa ligi kuu.
Aidha pia Emanuel Okwi na Godfrey Kaburu wamesimamishwa na uongozi huo kwa mda usiojulikana"
KAMA KWELI MMEMSIMAMISHA MPIGANAJI KABURU BASI HATA ILE NAFASI YENU YA PILI MSAHAU,AZAM WATAICHUKUA KIULAINI,ADEN NA KAMATI ZAKE ZA HARUSI HAWANA UBAVU KAMA KABURU
SAYZ MDAU WA BOMBA-GRAND RAPIDS,USA.