Makamu Mwenyekiti Simba SC ,
Geofrey Nyange (Kaburu) wa tatu kulia akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo
pichani),kuhusiana na KLABU ya soka ya Simba kuingia mkataba na kampuni ya
Prime Time Promotions Ltd unaohusiana na Promosheni na Masoko (Promotion and
Marketing) kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho (CAF) kati ya Simba na
Kiyovu Sport ya Rwanda. Kulia ni Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time
Promotions,Bw.Godfrey Mkama,Joseph Kusaga na shoto ni Katibu Mkuu wa Simba
Bw.Evodius Mtawali.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
KLABU ya
soka ya Simba ina furaha kubwa kuutangazia umma wa Watanzania kwamba imeingia
mkataba na kampuni ya Prime Time Promotions/Clouds Media Group unaohusiana na
Promosheni na Masoko (Promotion and Marketing) kwa ajili ya mechi ya Kombe la
Shirikisho (CAF) kati ya Simba na Kiyovu Sport ya Rwanda.
Ushirikiano huo wa namna ya kipekee una lengo la kuhakikisha kuwa
Watanzania wengi wanafahamu juu ya pambano hilo na wanahudhuria pambano hilo la
kimataifa lakini pia kuweka mazingira ya kuvutia kwa makampuni na
wafanyabiashara ili wawekeze katika mchezo huu kipenzi cha
Watanzania.
Ingawa
mkataba huu wa sasa baina ya Simba na Clouds unahusu mechi hii moja pekee, kuna
kila dalili kuwa huu utakuwa mwanzo wa kampuni hizi mbili kufanya kazi kwa
pamoja kwa muda mrefu kwa lengo la kuhakikisha mchezo wa soka unakua kwa faida
ya taifa letu.
Kwa
kuanzia tu, pamoja na mechi hii ya Kiyovu, Simba SC leo pia inatangaza kuanzisha
kwa luninga ya klabu, Simba TV, ambayo lengo lake kubwa litakuwa ni kuonyesha
shughuli za kila siku na matukio mbalimbali yanayohusiana na klabu
yetu.
Clouds
Media Group kupitia Clouds TV ndiyo watakaokuwa wakionyesha vipindi hivyo vya
Simba mara moja kwa wiki mwanzoni lakini lengo ni kuwa na televisheni ambayo
itakuwa inaonyesha habari za Simba saa 24 kila siku.
Ndiyo
maana basi, sisi katika Simba, tunaamini kuwa ushirikiano huu baina ya Simba na
Clouds unafungua njia ya maendeleo anuai katika kila nyanja inayohusiana na
mchezo wa soka hapa nchini.
Simba SC
inapenda kutumia fursa hii kukaribisha makampuni na wafanyabiashara kujitokeza
kudhamini mchezo wa soka hapa nchini kwa vile uzoefu unaonyesha kuwa kuwekeza
katika soka kunalipa.
Wenu
Katika Mapinduzi ya Soka Tanzania
Geofrey
Nyange
Makamu Mwenyekiti
Simba
SC