Mkuu wa Wilaya ya Moshi Alhaji Mussa
Samizi (kulia) akikabidhi zawadi ya Simu, fedha Tsh 80,000 na Mordem iliyo na
kifurushi cha kuanzia 20,000/= kwa mshindi wa pili wa mbio za Vodacom Fun Run,
Brazil Boay katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2012
zilizofanyika jana mjini Moshi. Katikati ni Mkuu wa Udhamini wa Vodacom, George
Rwehumbiza.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Alhaji Mussa Samizi (kulia)
akikabidhi zawadi ya Simu, fedha Tsh 80,000 na Mordem iliyo na kifurushi cha
kuanzia 20,000/= kwa mshindi wa tatu upande wa wanawake Natalia Elisante, wa
mbio za Vodacom Fun Run, Brazil Boay katika mashindano ya
Kilimanjaro Marathon 2012 zilizofanyika jana mjini Moshi. Katikati ni Mkuu wa
Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Alhaji Mussa Samizi (kulia)
akikabidhi zawadi ya Simu, fedha Tsh 100,000 na Mordem iliyo na kifurushi cha
kuanzia 20,000/= kwa mshindi wa kwanza upande wa wanawake Jackline Sakilu, wa
mbio za Vodacom Fun Run, Brazil Boay katika mashindano ya
Kilimanjaro Marathon 2012 zilizofanyika jana mjini Moshi. Katikati ni Mkuu wa
Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza.
Mmoja wa
washiriki walemavu alieshiriki katika mbio za kujifurahisha za
“Vodacom 5 KM fun run”akimaliza mbio zake.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Rukia Mtingwa wa
pili toka kushoto akifurahia jambo na baadhi ya watoto wenye ugonjwa wa ukimwi
mara walipomaliza kushiriki katika mbio za kujifurahisha za “Vodacom 5 KM fun
run”
Na Mwandishi Wetu, Moshi
Mbio za kujifurahisha za
kilometa 5 za (Vodacom 5KM fun run) ambazo ni sehemu ya mbio za
Kilimanjaro marathoni zimezidi kujizolea umaarufu kwa watu wengi
wa rika tofauti kujitokeza kushiriki kwenye mbio hizo zilizofanyika jana/leo
mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mahusiano wa kampuni ya
Mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wa mbio hizo, Rukia Mtingwa
katika mbio za mwaka huu jumla ya watu 10,000 wamejitokeza kushiriki kwenye mbio
hizo tofauti na makadirio ya kawaida ya kupata jumla ya washiriki
5000 ambacho ndicho huwa kiwango cha juu .
Mtingwa alisema wengi wa washiriki katika mbio hizo kwa mwaka
huu zimetokana na uhamasishaji mkubwa uliofanywa na vyombo vya
habari na mvuto wa mbio hizo ambazo huambatana na manjonjo mbalimbali
Kutoka kwa washiriki wake na zawadi za kuvutia zinatolewa na
Vodacom.
Pamoja na mafanikio hayo Mtingwa alisema wao kama wadhamini
wamepata changamoto kubwa katika mbio hizo hasa kwa mwaka huu
kutokana na wakimbiaji wazoefu kujitosa kushiriki kwenye mbio hizo
badala ya kuwaachia watu wengine ambao riadha sio fani yao .
“Kwa kweli mwaka huu tumekumbana na changamoto hiyo ya wakimbiaji
profession kushiriki kwenye fun run ambazo sisi tunaona ni maalum
kwa watu ambao riadhi si fani yao kwahiyo kipindi kijacho endapo tutaendelea na
udhamini wa mbio hizi itabidi tuifanyie kazi changamoto hii,”alisema Mtingwa
.
Aidha Mtingwa alisema changamoto ya kujitokeza washiriki wengi kwao
ni faraja kubwa na watajipanga kukubaliana na haki hiyo ili
kuendana na mazingira ya ukubwa wa mbio hizo kadiri
watu watakavyokuwa wakijitokeza.
Washindi wa mbio za jana/leo
kwa upande wa wanaume ni Gailet Ismail ambaye alichukua na nafasi
ya kwanza na kujinyakulia simu ya mkononi aina ya ZTE S- 501,muda wa maongezi wa
Sh 20,000, modem ya intaneti pamoja na M-Pesa ya Sh 100,000.
Brazil Boay alichukua nafasi ya pili na kuzawadiwa simu ,muda wa
maongezi,modem ya intanert na M-Pesa ya Sh 80,000 wakati mshindi
wa tatu alikuwa Fabiano Nelson ambaye naye alipata simu,muda wa
maongezi,modem na M-Pesa ya Sh 60,000.
Na upande wa wanawake washindi walikuwa ni Jackline
Sakilu,Catherine Iranga na Natalia Elisante ambao nao walijishindia zawadi sawa
na zile walizopata wanaume , washindi wengi kuanzia nafasi wanne
hadi 10 pamoja na wshiriki walioweza kumaliza mbio hizo nao walipata zawadi
mbalimbali kutoka Vodacom.
Huo ni mwaka wa tano tokea Vodacom iwe mdhamini wa
mbio za kilometa tano za kujifurahisha (Vodacom fun run) ambazo ni sehemu ya
mbio maarufu za Kilimanjaro ambazo mwaka huu zimeadhimisha miaka 10 tokea
kuanzishwa kwake .