JOH MAKINI, PROF.J KUPAMBA USIKU WA HIP HOP DAR LIVE MACHI 4

Wadau mbalimbali wa muziki wa Hip Hop hapa nchini, Jumapili ya Machi 4 mwaka huu wanatarajiwa kufurika ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kuhudhuria onesho kabambe la Hip Hop. Katika usiku huo wadau mbalimbali waliochangia muziki huu kufikia hapa ulipo watatunukiwa tuzo. Wakali wa muziki huo Profesa J na Joh Makini wamewawakilisha wasanii wenzao wa muziki huo katika mkutano wa kuthibitisha kushiriki tamasha hilo uliofanyika mchana huu ndani ya ofisi za Global Publishers zilizopo Mwenge jijini Dar.
Joh Makini kulia akizungumza katika mkutano huo katikati ni Meneja Mkuu wa Global Publishers na Mratibu Msaidizi wa tamasha hilo, Abdallah Mrisho kushoto ni Prof. Jay.

Post a Comment

Previous Post Next Post