MABINGWA wa soka Tanzania Bara Yanga
wamesema bado hawajaelewa mechi yao inachezwa wapi na lini baada ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kushindwa kuleta taarifa kwa wakati.
Yanga inayochea mechi yake ya marudiano na
Zalalek ya kuwania Kombe la Klabu Bingwa Afrika ambapo mechi yake ya kwanza
ilifanyika nchini Februali 18.
Katibu Mkuu
wa Yanga Mwesigwa Selestine, alisema kuwa mpaka jana hawajui wanachezea wapi na
tarehe ngapi.
Alisema kisheria taarifa zinatakiwa zifike
katika klabu yao kwa muda wa siku kumi kabla ya mechi lakini mpaka sasa kimya.
"Mpaka sasa wala hatuji wapi tunaenda
kucheza na ligi...maana hatujaambiwa chochote tunashindwa hata kutafuta kibali
(Visa) kwa wachezaji wetu ambao tunataka waende hiyo safari"alisema
Mwesigwa.
Alisema wao wamekuwa wakipata taarifa
kupitia mtandao hivyo aka hawajui nini wafanye.
Selestine alisema kama wataenda kucheza
Misri au nchi yoyote watakayoambiwa wataondoka Alhamis ya Machi mosi kwa kuwa
tayari wameshasikia kuwa mechi itacheza Jumamosi.
Akizungumza maandalizi ya mchezo yao Katibu
huyo wa Yanga alisema timu yao inaendelea vizuri na mazoezi chini ya kocha Mkuu
Kostadin Papic.
Selestine alisema hata mchezaji wao Yaw
Berko ambaye alikuwa nje muda mrefu ameanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo.
Alisema Berko yupo katika mazoezi ya pamoja
na wenzake hivyo maamuzi ya kwenda kwenyemechi yao ni ya kocha wao mkuu Papic
ndiye anaweze kusema kuwa anaqweza kucheza au la.
Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya
Zamalek hivyo inahitaji ushindi wa ugenini ili iweze kusonga mbele katika
mashindano hayo.