SIMBA TV YAJA, MASHABIKI WA AZAM NAO KAENI MKAO WA KULA


USHIRIKIANO ilioingia kampuni ya Prime Time Promtions na klabu ya soka Simba umelenga mambo mengi ikiwemo kuanzishwa kwa Simba Tv ambayo itazinduliwa rasmi Machi 4 wakati Simba itakaporudiana na Kiyovu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya Shirikisho barani Afrika (CAF).
 Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kwamba Simba Tv  itakuwa ikionyesha matukiao na taarifa mbalimbali zinazoihusu klabu ya Simba na kwa kuanzia itakuwa ikirushwa Clouds Tv mara moja kwa wiki kabla ya baadaye kuanza kurushwa katika moja ya televisheni za kulipia.
Naye Mkurugenzi wa Prime Time, Joseph Kusaga aliipongeza Simba kwa kukubali kwao mpango wao wa jitihada za kuendeleza soka nchini na kusema kuwa ushirikiano huo hautaishia kwa Simba tu bali hata kwa vilabu vingine pia.
“Tulishaahidi kuanzia mwaka 2012 tutasapoti michezo hivyo watanzania mtegemee kuona vitu vikubwa, vizuri na vyenye utofauti kupitia mchakato huu wa kuendeleza michezo nchini,”Alisema Kusaga.
Kusaga aliongeza kuwa pamoja na Simba, pia wapo katika mchakato kama huo kwa Azam Fc pia ambayo kama ilivyo kwa Simba Tv kutakuwa na Azam Tv itakayoanza kwa kurushwa katika kituo cha Clouds TV.

1 Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHFebruary 26, 2012 at 8:21 PM

    WIZI MTUPU...MI NILISHTUKA NIKIDHANI NI TV YA CLUB KWELI KUMBE WATAKUA NA KA KIPINDI KWA MWEZI MARA MOJA KWENYE TV YA CLOUDS?HIVI HIZI TIMU ZETU ZINASHINDWA NINI KUWA NA REDIO NA TV ZAO MPAKA ZIDANDIE DANDIE KWENYE MEDIA ZA WATU BINAFSI?TIMU KAMA SIMBA NA YANGA ZENYE MTANDAO WA MASHABIKI KILA KIJIJI TANZANIA ZILITAKIWA KUWA NA MEDIA HOUSE ZAO ZILIZO FULL SIO KUTUMIWA TUMIWA NA TV ZA WATU,HIZO TIMU ZENYEWE ZINAJIUZA NA RAHISI KUPATA SPONSORS WA KU RUN HIZO REDIO NA TV WHY ZIPITIE KWENYE TV NA REDIO ZA WATU-HAKUNA VIONGOZI,NA YANGA MKIFUATA UPUUZI HUU MTANIUDHI NA NCHUNGA NTAKUDHARAU ILE MBAYA NA USOMI WAKO,ENDELEENI NA MIPANGO ENDELEVU INAYOELEWEKA KAMA ULE MPANGO WENU WA KUINGIA MKATABA WA UJENZI WA JENGO LA YANGA PALE MTAA WA MAFIA N.K.ACHANENI HIZI CHEAP POPURARITY ZINAZOWAHANGAISHA VIONGOZI WA SIMBA KILA KUKICHA WANAKUJA NA JIPYA,SASA HIVI HAWAIMBI TENA HABARI ZA UWANJA WA KISASA WENYE MADUKA...NA WAANDISHI HAWAWAHOJI NA KUWAANIKA KWA MISIFA YA OVYO OVYO

    MDAU WA BOMBA LA UHURU,REVERE,MASACHESSETS,USA

    ReplyDelete
Previous Post Next Post