MECHI YA YANGA, ZAMALEK KUCHEZWA SAA
12
Mechi ya marudiano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika kati ya Zamalek na Yanga itachezwa Machi 3 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Jeshi jijini Cairo kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Misri.
Kwa mujibu wa maelekezo ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mechi hiyo itachezwa bila washabiki
kwa vile Zamalek inakabiliwa na adhabu ya kucheza mechi hiyo bila
washabiki.
Mechi hiyo itachezeshwa na
waamuzi kutoka Morocco ambao ni Jihed Redouane, Rouani Bouazza na Bekkali Mimoun
wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Gihed Greisha wa Misri. Kamishna wa mchezo huo
ni Ben Khadiga wa Tunisia.
WASOMALI KUCHEZESHA SIMBA,
KIYOVU
Mwamuzi i Yabarow Hagi Wiish
na wasaidizi wake Aweis Ahmed Nur na Abdirahman Omar Abdi, wote kutoka Somalia
ndiyo watakaochezesha mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na
Kiyovu Sport ya Rwanda.
Kwa mujibu wa orodha ya waamuzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), mwamuzi wa akiba kati mechi hiyo
namba 14 itakayochezwa Machi 4 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam atakuwa
Waziri Sheha wa Tanzania. Kamishna wa mechi hiyo ya raundi ya
awali atakuwa Jean Marie V. Hicuburundi kutoka Burundi.
CAF imeziingiza moja kwa moja
kati raundi ya kwanza timu 16 kutokana na ubora wake. Timu hizo ni ES Setif
(Algeria), Interclube (Angola), Asec Mimosas (Ivory Coast), Enppi (Misri), AS
Real Bamako (Mali), CO de Bamako (Mali) na CO Meknes (Morocco).
Nyingine ni WAC (Morocco),
Warri Wolves (Nigeria), Heartland (Nigeria), St. Eloi Lupopo (Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo- DRC), Us Tshinkunku (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-
DRC), El Amal Otbara (Sudan), Al Ahly Shandy (Sudan), CSS (Tunisia) na CA
(Tunisia).
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)