Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limeandaa kozi ya awali ya madaktari au wataalamu wa viungo
(physiotherapist) kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza itakayofanyika
jijini Dar es Salaam.
Kozi hiyo ya siku tano
itakayoanza Machi 5-9 mwaka huu itakuwa na washiriki 32 tu. Kila klabu inatakiwa
kutuma mshiriki mmoja ambapo anatakiwa kuwa daktari wa timu au
physiotherapist.
Katika sifa za kitabibu,
washiriki wanatakiwa wawe Clinical Officer (Medical Assistant), Assistant
Medical Officer na Medical Officer au Physiotherapist. Ada ya kushiriki ni sh.
60,000.
Washiriki wanatakiwa kutuma
TFF wasifu wao (CV) na nakala za vyeti vyao vya kitaaluma na mwisho wa
kuthibitisha kushiriki kozi hiyo ni Machi Mosi mwaka huu. Kwa madaktari
wanatakiwa wawe ambao kwa sasa wanazitumia klabu husika (active).
Kila klabu itamgharamia
mshiriki wake kwa malazi, nauli ya kuja na kurudi pamoja na posho wakati TFF
itatoa vifaa vya kozi (stationeries), chai na chakula cha mchana.