SHABAN KADO
UTATA kuhusu wachezaji wa Yanga waliopo timu
ya Taifa ‘Taifa Stars’ kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa
ya Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbiji, umemalizika baada ya kikosi cha Yanga
kutarajiwa kuondoka nchini Machi Mosi kwenda Cairo, Misri tayari kwa mechi yao ya
marudiano ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek ya huko.
Awali uongozi wa Yanga
ulipinga wachezaji wake waliopo Stars, Shaban Kado, Stephen Mwasika na Shadrack
Nsajigwa kucheza mchezo huo kwa madai ya kuhofia kupata muda wa kuungana nao
katika safari ya nchini Misri tayari kwa mechi hiyo itakayopigwa Machi 4.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam
jana kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinasema kuwa nyota Shaban Kado, Shadrack
Nsajigwa na Stephano Mwasyika wameruhusiwa kucheza mechi hiyo kutokana na ukweli
kwamba hakuta kuwa na safari ya mapema kama ilivyodaiwa awali baada ya kuwepo
kwa utata juu ya mechi hiyo.
Mmoja ya viongozi wa Yanga
alisema kwamba kutokana na kuwa na muda wa kutosha kabla ya safari hiyo hawana
umuhimu wowote wa kuwahi Misri hivyo hawana sababu ya kutowaruhusu wachezaji wao
ili kuitumikia timu ya Taifa.
Katika mchezo wa awali
ulipogwa jumamosi iliyopita katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, timu
hizo zilitoka sare ya bao 1-1.