Na Dina Ismail
WAKATI mgomo
baridi miongoni mwa wachezaji wa Simba ukipatiwa ufumbuzi kwa Makamu Mwenyekiti
wa klabu hiyo Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kuokoa jahazi, uongozi wa klabu hiyo
umemtema katika safari ya Algeria kiungo wake wa kimataifa, Patrick Mutesa
Mafisango.
Wachezaji wa
Simba waliendesha mgomo wa chini chini kwa karibu siku tatu, wakishinikiza
walipwe sh mil. 30 walizoahidiwa na uongozi - iwapo wangeifunga ES Setif ya
Algeria, waliyocheza nayo Jumapili iliyopita katika mechi ya awali raundi ya
kwanza ya Kombe la Shirikisho (CAF) kwenye Uwanja wa Taifa na kuibuka na
ushindi wa mabao 2-0 na kuambulia sh milioni 15 tu.
Habari kutoka
katika kambi ya klabu hiyo iliyoko Bamba Beach, Kigamboni jijini Dar es Salaam
zinaeleza kuwa Kaburu alikwenda kambini na kuwaongeza shilingi milioni tano na
hivyo kuamua kuachana na mgomo huo.
Imeelezwa kuwa
pamoja na mgao huo, kulifanyika kikao juzi jioni ambapo wachezaji waliamua
kuuzika mgomo huo na kujipanga kikamilifu tayari kwa mchezo wao wa Ligi Kuu
Tanzanuia Bara dhidi ya African Lyon utakaopigwa kesho katika dimba la Taifa
Dar es Salaam na ile ya marudiano dhidi ya ES Setif itakayopigwa wiki mbili
zijazo.
Aidha suala
hilo la kudai malipo hayo pia lilipelekea Mafisango kusimamishwa, baada ya
kurejea kambini akiwa amelewa na kuanza kumtolea lugha chafu Meneja wa Timu
hiyo, Nico Nyagawa, kabla ya kutaka kumpiga Kocha Mkuu, Mserbia Milovan
Cirkovic, yote ikiwa ni katika kudai maslahi ya timu hiyo.
Habari zinadai
kuwa katika vurumai hiyo, Mafisango aliulalamikia uongozi wa Simba kutojali
maslahi ya wachezaji, huku akimshutumu Nyagawa kwa kushindwa kuwatetea pindi
walipotaka waongezewe mgao wao. Hata hivyo Mafisango alikuwa hajajua kama
tayari wameshaongezwa milioni tano.
Tayari uongozi
wa Simba umempa barua ya kumsimamisha kuichezea timu hiyo kwa muda, sambamba na
kumtaka ajieleze kutokana na kufanya utovu wa nidhamu kwa waajiriwa wengine wa klabu hiyo katika kambi
ya timu hiyo.
Taarifa
iliyotolewa leo na Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga ilisema kuwa kutokana
na utovu huo wa nidhamu, Mafisango hatasafiri na timu kwenda Algeria wiki ijayo
itakapoenda kukwaana na Setif ya huko katika mchezo wa marudiano.
“Uongozi tayari
umemuandikia barua ya kutaka ajieleze kwa makosa yake na maamuzi kamili
yatatolewa mara timu itakaporejea kutoka Algiers,” ilieleza taarifa hiyo.
Mafisango is a disaster,ni mchezaji mzuri sana lakini hanaga nidhamu,hata azam aliwahi kumtukana kocha mbrazil siku wakiwa safarini kutoka Dodoma kuja Dar kisa yeye na mwenzake nimemsahau jina ila aliwahi kuchezea ashanti akaja simba then ndio akaenda azam nadhani ni kijuso au lidondo walicheza mechi dodoma ilikua jmosi usiku wao wakasema wanaenda disco kocha akawaambia wachezaji timu itaondoka dodoma jpili saa kumi na moja alfajiri hivyo ni bora wachezaji wakapumzika kwa kulala mapema kujiandaa na safari but hamkatazi mtu kutoka ila azingatie muda wa timu kuondoka na kuwahi,kina mafisango wakaenda disco wakachelewa saa kumi na moja kamili kocha akamwambia dereva ondoa gari,kina mafisango ikabidi wakodi teksi kulifukuza basi la timu baada ya kukuta limeondoka,bahati nzuri wakalikuta njiani,basi baada ya kuingia ndani ya basi mafisango akaanza kumporomoshea matusi kocha mbrazil na viongozi wote wa timu na kudiriki kutaka kumpiga,kocha akaapa akifika dar ama yeye aachie ngazi au mafisango aachie,viongozi wa azam wakawa dhaifu kwa mafisango wakaona bora kocha aondoke..huyo ndio mcongoman mafisango ambae amaechukua uraia wa rwanda...ankunywa sana pombe,anavuta sana bangi..!
ReplyDeletemdau wa bomba revere,boston,massachussetts.