MKAKATI wa uundwaji wa kampuni ya kusimamia Ligi Kuu ya
Tanzania Bara umefufuliwa leo kwa kikao kilichofanyika kwenye hoteli ya JB
Belmonte katikati ya Jiji ya Dar es Salaam.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti Geoffrey
Nyange 'Kaburu' na Katibu Celestine Mwesigwa, klabu 10 zilihudhuria na nne tu
viongozi wake hawakuweza kufika ambazo ni Ruvu Shooting, JKT Oljoro, Kagera
Sugar na Mtibwa Sugar.
Klabu zimefikia mwafaka wa kumuagiza mwakilishi wa Coastal
Union ya Tanga, Wallace Karia ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati yua Utendaji ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwsilisha hoja zao kwa Kamati ya Utendajiya
TFF, ili suala lao lijadiliwe katika Mkutano Mkuu, utakaofanyika Machi 24,
mwaka huu.
Ligi Kuu inaendeshwa na TFF, lakini klabu zinataka TPL ianze
kuendesha ligi hiyo kuanzia msimu ujo na msimamo ulikuwa mkali katika kiko cha
leo.
Klabu zitakutana tena Jumapili ili kumalizia mchakato wa
hoja zitakazowasilishwa na Karia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi Kuu
iliyoundwa na TFF kwenye Kamati ya Utendaji ya TFF.
MBONA HAYASOMEKI,REKEBISHENI HALI HII INASABABISHA USUMBUFU NAONA KAMA MNAANZA KUIZOEA NA KUIONA YA KAWAIDA
ReplyDelete