Tukio hilo linakuja baada ya
hivi karibuni wachezaji wa Kikwajuni kumshushia kipigo cha aina yake, mwamuzi
Waziri Sheha.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi kwa njia ya simu kutoka Zanzibar jmchana Msemaji wa ZFA, Munir
Zakaria, alisema kuwa uamuzi huo umetolewa jana baada ya kikao cha kamati
tendaji ya ZFA iliyoketi kujadili kitendo hicho kilichotokea juzi.
Alisema baada ya kupitia
ripoti ya mwamuzi na ile ya kamisaa na kuwasikiliza wahusika, ZAFA iliamua
kutumia kanuni ya 25 inayozungumzia adhabu zinazostahili kutolewa kwa
wanaowapiga waamuzi na ikizingatiwa kuwa vitendo hivyo vinataka kukithiri
katika soka la Zanzibar.
“Baada ya kuona vitendo vya
kuwapiga waamuzi vinakithiri katika viwanja vya soka Zanzibar kamati tendaji ya
ZFA iliyoketi leo asubuhi ‘jana’ imeamua kuishusha kwa madaraja mawili kwa
mujibu wa kifungu cha sheria ibara ya 25, imewafungia viongozi wake wote mwaka
mmoja, pamoja na wachezaji pia wote watatakiwa kulipa faini ya sh 100,000 kila
mmoja,” alisema Zakaria.
Aliwataja wachezaji
waliofungiwa kwa mwaka mmoja na kutozwa faini ya sh 100,000 kuwa ni Njema
Francis, Khatibu Hussein, Idi Kambi, Khalid Shaame, Ahmed Omari, Hassan
Ramadhani na Abdallah Omari, ambao ndio waliobainika kuwa.
Zakaria aliwaonya viongozi wa
klabu, wachezaji na mashabiki kuacha tabia ya kuwapiga waamuzi badala yake
akawataka kukata rufaa au kuwasilisha mamalalamiko yao kwa maandishi iwapo wana
malalamiko dhidi ya waamuzi na ZFA itayafanyia kazi mara moja.