VINARA wa ligi kuu bara na wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye
michuano ya
Kimataifa Simba, wameingia kambini leo kujiandaa na
michezo yake ligi hiyo
na ile ya kimataifa.
Simba imengia kambini baada ya kushinda mechi yake
ya kombe la
Shirikisho (CAF) jumapili iliyopita dhidi ya Es Setif ya Algeria
kwa
mabao 2-0 katika mechi iliyopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar
es
Salaam.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema kikosi chote
cha Simba
kimeingia kambini katika hoteli ya Bamba Beach iliyopo
Kigamboni
jijini Dar es Salaam na itakuwa ikifanya maandalizi yake huko
huko.
Alisema wachezaji wote wapo katika hali nzuri na ari ya kufanya
vema
katika michezo yao ya hivi karibuni wakianza na ule wa ligi kuu
bara
dhidi ya African Lyon jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa.