KATIBU Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah
amesema
anamshukuru mungu kwa kuwawezesha madaktari bingwa wa upasuaji
nchini India
kumpatia matibabu mazuri na hatimaye kurejea salama
nyumbani.
Kabla ya
kwenda huko Osiah alilazwa katika kitengo cha Taasisi ya Tiba
ya Mifupa (MOI)
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, baada ya
kubainika kuwa ana uvimbe
kichwani kwake na hivyo kushauriwa kwenda
nchini India.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo alisema kwa sasa anaendelea
vizuri ingawa wakati wa
zoezi hilo alipata maumivu makali ya macho
yaliyotokea wakati akifanyiwa
upasuaji kwani sehemu kubwa ya paji
la uso ilivutwa ili kupata uwiano mzuri
wakati wakimshona nyuzi.
Alisema mara baada ya upasuaji huo madaktari
walimueleza kuwa uvimbe
uliota nje ya ubongo na ndiyo kitu cha kushukuru
inagwa ulipoaanza
kugusa ubongo ndio tatizo likaanza na ndio maana hakuwa
katika hali ya
kawaida.
Angetile alisema baada ya kumaliza uangalizi
maalum aliopewa nchini
humo madaktari hao wamemtaka kwenda katika hospitali
ya Aga Khan
baada ya mwezi mmoja ili kuangalia maendeleo ya afya
yake.
“Zoezi la kwenda Aga Khan litakuwa wiki ijayo ila kwa
sasa
nashughulikia mapumziko mafupi ya kama wiki mbili hivi ili
niweze
kupumzika zaidi,”Alisema Osiah.