SIMBA
SPORTS CLUB
WEBSITE www.simba.co.tz|
AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA
29/03/2012
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Wasalaam.
KLABU ya Simba inapenda kutoa
taarifa zifuatazo kwa vyombo vya habari.
SUALA LA MAFISANGO
Mchezaji Patrick Mafisango
amesimamishwa kuichezea Simba kwa muda usiojulikana baada ya jana kufanya
vitendo vya utovu wa nidhamu kwa waajiriwa wengine wa klabu na klabu kwa ujumla
katika kambi ya timu iliyopo Bamba
Beach jijini Dar es
Salaam.
Kutokana na utovu huo wa nidhamu, Mafisango hatasafiri na timu kwenda
Algeria. Uongozi tayari umeamuandikia barua ya kutaka ajieleze kwa makosa yake
na maamuzi kamili yatatolewa mara timu itakaporejea kutoka Setif kwenye mechi
ya marudiano.
SUALA LA MGOMO
Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti wiki hii kuwa wachezaji wa Simba
wapo katika mgomo kutokana na kutopewa stahili ya mgawo wao wa mapato kwenye
mechi dhidi ya Setif.
Taarifa hizi hazina ukweli wowote. Kwanza, wachezaji karibu wote wa
Simba isipokuwa wale ambao taarifa zao zinajulikana kwa uongozi wako kambini.
Wachezaji wa Simba wasingeweza kugomea mgawo huo kwa sababu mikataba yao
inaeleza wazi kuwa wanatakiwa kulipwa asilimia ya mapato ya mechi kwenye mechi
za ndani na si zile za kimataifa.
Tunakaribisha waandishi wa habari na vyombo vyao waje kambini Bamba na
wajionee wenyewe kwa macho yao kama kuna hicho kinachoitwa MGOMO.