KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imemwaga zaidi ya Shilingi 15
bilioni kuidhamini timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kwa muda wa
miaka mitano.
Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu vya habari, zinasema
kuwa siku chache zijazo TBL na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watasaini
mkataba huo mkubwa na aina yake kuwahi kutokea nchini.
Habari za uhakika zinasema kuwa TBL imekubali kuidhamini
Taifa Stars kwa Shilingi tatu bilioni kila mwaka hivyo kwa miaka mitano itakuwa
Sh.15 bilioni.
Huu utakuwa ni udhamini mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika
historia ya soka nchini.
Hakuna upande uliokuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani pande zote
zinataka kufanya hafla ya nguvu wakati wa kusaini mkataba huo mbele ya vyombo
vya habari.
Siku chache zilizopita TFF ilitangaza kuwa haitaongeza
mkataba na wadhamini wao wa zamani Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) ambao kwa
miaka mitano walioidhamini Taifa Stars kulikuwa na msisimko mkubwa wa soka.
CHANZO:Shaffih blog