IDADI kubwa ya wachezaji ambao umri umewatupa mkono ndani ya
klabu ya Inter Milan
ya Italia ndio chanzo cha kushuka na kwa Mabingwa hao wa Ulaya mwaka 2010 hadi kutolewa kwenye Ligi ya
Mabingwa na Olympique Marseille ya Ufaransa.
Rais wa klabu hio Massimo Moratti alimuondolea makosa kocha
Claudio Ranieri kufuatia mchuano wa jumanne kutokana na magoli ya ugenini.
Mchuano huo ulimalizika 2-2 baada ya Inter kushinda nyumbani
2-1, lakini bao la ugenini likabadili matokeo na hivyo kuashiria kua Inter
msimu huu inaondoka kapa bila Kombe hata moja.
Klabu hio imeisha ondolewa katika
mashindano ya Kombe la Italia ikiwa ya saba kwenye msimamo wa Ligi ya Serie A.
Hali hii ilianza punde baada ya kocha wao Jose Mourinho
kuondoka kufuatia ushindi wa makombe matatu miaka miwili iliyopita.
Mreno huyo mjanja alifahamu vyema umri wa kikosi cha Inter
kua hautoiwezesha kufikia kiwango hicho tena na kuondoka na heshima yake.
Rafa Benitez akafuata kujaribu bahati yake, akashindwa na
Leonardo akamrithi naye akianguka, kisha akaja Gian Piero Gasperini na baada ya
kushindwa ndio akateuliwa Ranieri.
Rais wa Inter amesema haifai kufikiria mageuzi bali ni
marekebisho.Sidhani kama kocha ana tatizo,
angalau hadi mwisho wa msimu.