MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga leo
watakuwa na kazi moja tu ya kusaka pointi tatu kupitia mchezo wao na Villa Squad utakaopigwa katika Uwanja wa
Taifa, imefahamika.
Ofisa habari wa Yanga
Louis Sendeu alisema kikosi chake kipo
katika hali nzurti na wamejipanga vema kuhakikisha wanashinda mechi hiyo ili
kujiweka katiika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao.
“Unajua sasa hivi ni kipindi chja lala salama hivyo ni
lazima tujipange vema na kuhakikisha tunashinda mechji zetu zilizobaki huku
tukiwaombea mabaya wale walio juu yetu…yote kwa yote tumejipanga vema
kuhakikisha malengo yanatimia,”alisema SEndeu.Viingilio katika mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Oden Mbaga mwenye beji ya Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA) vitakuwa shilingi 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, shilingi 5,000 kwa watakaokaa viti vya rangi ya chungwa, shilingi 10,000 kwa VIP C na B na shilingi 15,000 kwa VIP A.
Mbali ya mechi ya Yanga na Villa, leo pia kutakuwa na mchezo mwingine wa ligi hiyo utakaozikuytanisha Coastal Union na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.