Shukrani
Familia ya Eng. Gabriel Mponzi wa Oyster Bay na familia ya
marehemu Dr.Allan Makange wa Kibaha
Dar-es-salaam zinapenda kutoa
shukrani zake za dhati kwa wote walioshirikiana nao kwa namna moja au nyingine
kwenye kipindi kigumu cha msiba na kuhitimisha safari ya mwisho ya mpendwa wao
Jane Mkami Mponzi.
Ni vigumu kutaja mtu mmoja
kuwa ndiye aliyekuwa na msaada
zaidi, ila hatuna budi kutoa shukrani zetu kwa madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya Aga Khan kwa jitihada zao za kuokoa maisha ya
Jane. Maparoko na mapadre wa kanisa katoliki la Mt. Petro Oyster Bay, Dar Es Salaam pamoja na wale wa Ipamba
Iringa na wanakijiji wake wote. Jumuiya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ya Oyster Bay Dar Es Salaam; IPP Media;
Vodacom Tanzania; Africa
Media Group; wamiliki
wa blog mbalimbali Tanzania; majirani na
marafiki zetu wote, asanteni sana.
Shukrani yetu kubwa
ni kwa Mungu Mwenyezi kwa kutupatia zawadi
ya maisha ya Jane
hapa duniani, na tutaishangilia zawadi hii kwa kumsifu na kumtukuza Mungu siku zote za maisha yetu.
Tunapenda
kuwakaribisha wote kwenye mkesha maalum wa kuyaenzi maisha ya Jane tarehe 13 Aprili 2012 kuanzia saa 11 jioni nyumbani
kwa Eng.Mponzi #39, Br. Msasani,
Oyster Bay. Pia kutakuwa na Misa ya
shukrani kwenye kanisa la Mt. Petro Oyster Bay siku ya Jumamosi 14 Aprili
kuanzia saa 12.30 asubuhi na baadae tutamalizia na chai nyumbani Oyster
Bay. Wote mnakaribishwa
sana.
“Kwa maana sisi,
wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka
huko tena tunamtazamia mwokozi, Bwana Yesu
kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa
utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe
chini yake” Wafilipi 3:20-21